Sibuka FM

Bariadi dc yaomba kutumia bilioni 34 mwaka wa fedha 2025/26

8 January 2025, 8:53 pm

Kwenye picha ni mkuu wa wilaya ya Bariadi,Simon Simalenga akiwa kwenye moja ya shughuli za kimaendeleo Picha ni kwa hisani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bariadi

Uroho wa viongozi kutaka maendeleo katika maeneo yao ya kiutawala ni chachu moja wapo ya kutambua kiongozi mwenye kujali wananchi anaowaongoza”.

Na, Daniel Manyanga

Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga amewashauri madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi kuzingatia usawa katika mgawanyo wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata za halmashauri hiyo ili kuleta usawa wa maendeleo katika maeneo hayo.

Simalenga ametoa ushauri huo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, kilichoketi kwa ajili ya kujadili na kupitisha rasimu na mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo amekemea tabia ya baadhi ya madiwani kwenda kinyume na maamuzi ya baraza la madiwani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kudhani kuwa wao katika maeneo yao ya kiutawala wanasitahili kupewa mgawanyo mkubwa zaidi ya wengine.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bariadi,Simon Simalenga akizungumzia kuwepo kwa usawa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Kwenye picha aliyesimama ni mwenyekiti wa baraza la madiwani wilaya ya Bariadi dc,Mayala Lucas Picha ni kwa hisani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bariadi

Akizungumza kwenye baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mayala Lucas, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwenye suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuahidi kulisimamia suala hilo kama ilivyoshauriwa na mkuu wa wilaya ili kuleta usawa wa maendeleo katika kata zote wilayani hapo.

Sauti ya mwenyekiti wa baraza la madiwani wilaya ya Bariadi vijijini akielezea uwepo wa viongozi hao

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi amefafanua kuhusu rasimu na mpango wa bajeti uliopitishwa na baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na kutaja makisio ya ukusanyaji wa mapato katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Sauti ya mwenyekiti wa baraza la madiwani wilaya ya Bariadi DC ,Mayala Lucas akitolea ufafanuzi makadirio ya mapato na matumizi mwaka wa fedha 2025/26