X-ray yapunguza gharama na muda wa matibabu wilayani Maswa
17 December 2024, 9:30 pm
” Umbali na gharama za kufuata huduma ya mionzi katika wilaya jirani ulikuwa kikwazo kwa wananchi wenye kipato cha chini lakini kusogezwa kwa huduma hiyo karibu kwa wananchi kumeleta faraja.”
Na, Daniel Manyanga
Wananchi wilayani Maswa mkoani Simiyu wamefurahia ujio wa mashine ya mionzi(X-ray) katika hospitali ya wilaya hiyo hali ambayo itapunguza muda na gharama waliokuwa wanatumia kufuata huduma ya mionzi wilaya ya Bariadi hadi nje ya mkoa wa Simiyu.
Wakizungumza na Sibuka fm baadhi ya wananchi walioshuhudia ufungaji wa mashine ya mionzi(X-ray) katika hospitali ya wilaya ya Maswa wamesema kuwa ujio wa huduma hiyo utasaidia kupunguza gharama na muda ambao walikuwa wanaotumia wakati wa kufuata huduma ya mionzi katika wilaya ya Bariadi hadi nje ya mkoa huo huku wakimshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta huduma hiyo.
Dr.Hadija Zegega ni mganga mkuu wa wilaya ya Maswa amesema kuwa kabla ya ujio wa X-ray wagonjwa walikuwa wanasafiri kwa umbali mrefu kufuata huduma hiyo huku wakipunguza gharama za kiutendaji pamoja na kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi.
Akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya wilaya hiyo pamoja na wananchi baada ya kufungwa kwa mashine ya mionzi (X-ray) mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amemtaka mkandarasi kukabidhi mradi huo mara moja ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo.