Bil 2.9 zatolewa na serikali kukarabati chuo cha maafisa tabibu Maswa
1 December 2024, 11:10 am
Chuo hiki kinaenda kubadilika kabisa na kuwa kipya kwani Rais wenu ametoa Fedha zaidi ya Bilioni 2. 9 ili kufanya Ukarabati wa Miundombinu, Niwahakikishie tu nyie Wahitimu mkirudi hapa Mwezi Juni mwakani mtakuta Mazingira tofauti kabisa, mtatamani mrudi kusoma hapa tena ” Dkt Godwin Mollel Naibu Waziri wa Afya”
Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa Fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 2. 9 kwa ajili ya Kukarabati chuo cha Maafisa Utabibu Kilichopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu
Dkt Mollel amesema hayo wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa chuo hicho pamoja na Mahafali ya 48 yaliyofanyika chuoni hapo na kuongeza kuwa hadi kufikia mwezi Juni, 2025 Ukarabati huo utakuwa Umekamilika
Akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge amesema kuwa kumekuwepoo na Mapinduzi Makubwa katika Sekta ya Afya ambapo wa sasa Wilaya ina Vituo vya Afya 6 ikilinganishwa na hapo awali kabla ya Rais Samia hajaingia Madarakani kulikuwa na Vituo vya Afya 3 tu.
Awali akitoa Risala kwa Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha Maafisa Tabibu Dr Hangwa Enos Hangwa amesema kuwa kuwekuwepo na Changamoto ya Uchakavu wa Miundo mbinu ya Majengo hivyo kuiomba Serikali kukiboresha Chuo hicho
Baadhi ya Wazazi walioshiriki sherehe hiyo ya Miaka 50 ya kuanzishwa kwa chuo na Mahafali ya 48 wamemshukuru Mh Rais kwa kutoa Fedha hizo kwa ajili ya Ukarabati ili kiendane Mazingira ya sasa