Kipindupindu ni zaidi ya vita Simiyu, Amref watia nguvu
19 November 2024, 8:53 pm
“Adui wa maendeleo ni maradhi hatuwezi kufanya kazi za kiuchumi wakati huo wananchi wanachangamoto ya kiafya hivyo jukumu letu ni usalama kwanza wa raia”.
Na, Daniel Manyanga
Shirika la Amref Heath of Africa chini ya mradi wa Afya Thabithi unatekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Tanzania Communication Development Center (TCDC) limewataka wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu kuendelea kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa huo.
Akizungumza na Sibuka fm wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu afisa elimu ya mabadiliko ya tabia kutoka shirika la Tanzania communication development center (TCDC ) mkoani Simiyu,Antony Nakasenga amesema kuwa ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo wananchi wanapaswa kuepuka kunywa maji yasiyo salama, kutumia vyombo safi na kuhakikisha wanakula chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi pamoja na matumizi ya vyoo.
Kwa upande wake mhamasishaji wa maswala ya mabadiliko ya kitabia katika jamii mkoani wa Simiyu,Maria Masanzu amewataka wananchi kuhakikisha wanawapitia huduma ya kwanza kwa wagonjwa ikiwemo kuwatengenezea Glucose ama olo endapo kama kuna mtu katika familia ataonekana kuwa na dalili moja wapo kati ya Kuhara na Kutapika bila tumbo kuuma na baada ya hapo wampekeke katika vituo vya afya au hospitali kwa matibabu zaidi.
Kipindupindu ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na bacteria aina ya Vibrio Cholera kupitia maji machafu au chakula kichafu(kula mavi mabichi).