Sibuka FM

Maswa:Kanda ya ziwa kinara kwa uharibifu wa mazingira

8 November 2024, 4:00 pm

Pichani ni afisa mazingira wilayani Maswa,Dutu Lubinza akizungumza na wanawake na Samia hawapo kwenye picha katika hafra ya kuhimiza matumizi ya nishati safi Picha na Alex Sayi

Wakati dunia inapambana na mabadiliko ya tabia nchi utokanao na uharibifu wa mazingira haswa katika matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kanda ya ziwa kinara kwa uharibifu wa mazingira”.

Na, Daniel Manyanga

Zaidi ya hekta laki nne hupotea nchini Tanzania kutokana shughuli za kibinadamu za ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia na matumizi mengine.

Picha ikionesha namna ambavyo wanadamu wanavyoharibu misitu kwa matumizi ya kuni na mkaa Picha ni kutoka maktaba ya Sibuka fm

Takwimu hizo zimetolewa na afisa mazingira wilayani Maswa,Dutu Lubinza wakati wa hafra ya wanawake na Samia wa mkoa wa Simiyu lililolenga kutangaza miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kuwahimiza wakinamama matumizi ya makaa ya mawe ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Dutu Lubinza amesema kuwa kwa mwaka nchini Tanzania zaidi  hekta laki nne na sabini hupotea kutokana na shughuli za ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa ili kupikia.

Sauti ya afisa mazingira wilayani Maswa,Dutu Lubinza akizungumza na wanawake na Samia ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Dutu amesema kuwa asilimia 20 ya uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti unatokea katika ukanda wa ziwa Victoria katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Kagera na Simiyu hivyo kufanya kuwa tishio katika miaka ya hapo badae kama hakutakuwa na juhudi zozote za kunusuru hali hiyo huenda kukawa na jangwa.

Sauti ya Dutu Lubinza akizungumzia namna ambavyo ukanda wa ziwa ulivyokuwa kinara wa uharibifu wa mazingira kutokana na matumizi ya kuni na mkaa

Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeshaandaa mpango kazi wa kumaliza matumizi ya kuni na mkaa kwa kutumia nishati safi itokanayo na matumizi ya makaa ya mawe,majiko ya gesi pamoja na kuandaa makongamano ya kuhimiza wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya afisa mazingira wilayani Maswa akielezea mipango ya serikali katika kumaliza matumizi ya kuni na mkaa
Muonekano wa picha zikionesha namna ambavyo shughuli za kibinadamu zinavyoharibu uoto wa asili pamoja na misitu picha kutoka maktaba ya Sibuka fm