Maswa: Wanawake na Samia waaswa kutumia nishati safi yakupikia
7 November 2024, 11:08 am
Matumizi ya nishati safi yakupikia inatajwa kuwa ni mwarobaini wa kukabiliana na uharibifu wa mazingira,huku ikitajwa kuwanufaisha wanawake Mkoani Simiyu kwakuokoa gharama,muda na maradhi yanayotokana na matumizi ya mkaa na kuni
Na,Alex Sayi
Wanawake na Samia mkoani Simiyu wameaswa kuunga mkono juhudi za Rais Samia,kwa kuchangamkia fursa ya matumizi ya Nishati safi yakupikia hususani makaa ya mawe hali itakayosaidia kunusuru uharibifu wa mazingira.
Hayo yemesemwa na mwenyekiti wa Wanawake na Samia mkoani Simiyu Bi,Mwanahawa Abdalla Said kwenye hafra ya Wanawake na Samia iliyofanyika Novemba,05,mwaka huu kwenye Ukumbi wa Halmashuri Wilayani Maswa.
Awali Bi,Said akizungumzia na Wanawake hao zaidi ya miatatu waliojitokeza kwenye hafra hiyo ya Wanawake na Samia alisema kuwa lengo la hafra hiyo nikumuunga mkono Rais Samia nakuisemea miradi yakimkakati inayotekelezwa chini ya utawala wake.
Kwa upande wake Katibu wa Wanawake na Samia Mkoani hapa,Bi,Hawa Issa Kilima amesema kuwa wameleta fursa hiyo ya matumizi ya nishati safi ya mkaa wa wawe kwa lengo la kutunza mazingira.
Akizungumza na wanahafra hao Afisa mazingira Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Bw,Dutu Kafula amesema kuwa matumizi ya nishati safi yakupikia yanalengo la kuepusha uharibifu wa mazingira.
Aidha kwa upande wao baadhi ya washiriki wa hafra hiyo Bi,Rehema Sabuni na Bi,Mwanahawa Abdalla Mwanzalima wakizungumza na Sibuka fm,wamesema kuwa wanafurahia ujio wa fursa hiyo kwakuwa itawapunguzia adha ya matumizi ya mkaa na kuni.