Maswa:Wanawake wahimizwa kuchota mafedha Halmashauri
7 November 2024, 9:23 am
Wakazi wilayani Maswa Mkoani Simiyu mbioni kunufaika na mikopo ya 10% inayotengwa na Halmashauri kutoka kwenye mapato yake ya ndani baada ya Serikali kusitisha zoezi hilo toka April,2023/2024.
Na,Alex Sayi
Wanawake na Samia wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamehamasishwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri kwa ajiri ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Simiyu Bi,Mwanahawa Abdalla Said,kwenye halfa iliyofanyika Novemba,05/2024kwenye Ukumbi wa Halmashauri Wilayani hapa
Bi,Said amewataka wanawake hao kuunda vikundi ili waweze kunufaika na fursa za mikopo zinazotolewa na Halmashauri na taasisi zingine za mikopo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Divission ya maendeleo ya jamii wilayani hapa Bw,Rogers Limo amesema kuwa tayari Halmashauri imeshatenga zaidi ya Shillingi,Mill,300 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake,vijana na watu wanye ulemavu
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii wilayani hapa Bi,Lucia Misinzo amesema kuwa tayari dirisha la kupokea maombi ya mikopo limeshafunguliwa huku akibainisha kuwa maombi hayo yataanza kuchakatwa kwenye kamati za mikopo katani.