Wanafunzi Masela sekondari wafundwa elimu ukatili wa kijinsia
24 October 2024, 11:04 pm
Jamii ya watanzania imeendelea kukumbushwa kuchukua tahadhari juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia,kwakutoa taarifa nakuendelea kuwaelimisha watoto walio majumbani na wanafunzi ili kuwanusuru watoto hao na athari za ukatili wa kijinsia.
Na,Alex Sayi.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Masela iliyopo kijiji na kata ya Masela wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamepatiwa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na athari zake kutoka shirika la Juniors and Child Care foundation (JACCAFO)
Elimu hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shirika hilo,Bw,Joseph Ngeleja wakati akizungumza na wanafunzi hao,baada yakudhuru shuleni hapo,Oct,21,mwaka huu kwa lengo la kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.
Awali Mkurugenzi huyo akizungumzia wasifu wa Shirika hilo amesema kuwa shirika hilo limejikita kusaidia watu wenye ulemavu,watoto waishio kwenye mazingira magumu,wanawake na wazee.
Emmanuel Cosmas mwanachama wa Shirika hilo akizungumza na wanafunzi hao amewataka wanafunzi hao kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia nakujiepusha na tamaa za muda mfupi.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa shule hiyo Msafiri Mageuza alimshukuru Mkurugenzi wa shirika hilo kwakufika nakutoa elimu hiyo shuleni hapo.
Aidha Claudia Macha na Benedicto Gitambi Gagagaga wakizungumza na Sibuka fm wamesema kuwa masuala hayo ya ukatili wa kijinsia yamekuwa na athari kwenye jamii hasa kwa watoto wa kike.