Wananchi Maswa walalamikia umeme kufika maeneo ya mijini tu
27 September 2024, 11:06 pm
“Unakuta meme umefika maeneo ya sentani tu halafu sisi tuliopo pembezoni hatupati tunaambiwa tu mradi unaishia hapo kwani sisi wa pembezoni hatustahili kupata huduma ya umeme?“
Wananchi wa kijiji cha Mwakabeya kata ya Ipililo Wilayani Maswa Wamelalamikia Huduma ya Umeme kufika kwenye Senta tu na wengine waliopo Maeneo ya Pembezoni kukosa Nishati hiyo Muhimu.
Wakitoa Kero hiyo Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Kenani Kihongosi baadhi ya wananchi hao Maduhu Tungu na Dogani Ndoma Lyabita wakapaza sauti zao na kuomba kusaidiwa ili nao wanufaike
Akitoa Majibu kuhusu Changamoto hiyo Meneja Tanesco Mkoa wa Simiyu Alistidia Clemence Kashemeza amekiri kuwepo Changamoto hiyo na kuahidi kukamilisha maeneo ambayo hayajafikiwa na Nishati ya Umeme huku akiwataka Wananchi kulinda na kutunza Miundombinu hiyo kwani Serikali inatumia gharama kubwa kuwafikia.
Kenani Kihongosi ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi Wanasogezewa Huduma mbalimbali ikiwemo Suala la Umeme hivyo wawe na subira katika kuiamini Serikali kuwa itawaletea huduma hiyo.
Mhe Kihongosi ameongeza kuwa katika Siasa ni vizuri kuvumiliana na Kupendana na siyo kuleta chuki zitakazopelekea kuharibu Amani tuliyonayo kwani kuna Maisha baada ya Siasa