Sibuka FM

Madereva wazembe,vyombo vibovu hakuna atakae kuwa salama Simiyu

19 July 2024, 5:29 pm

Pichani ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP, Edith Swebe picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

“Katika kuzuia na kupambana na madereva wazembe  wanaosababisha ajali zisizo za lazima zinazotokana na ubovu wa vyombo vya usafirishaji wanavyotumia jeshi la polisi mkoa wa Simiyu limekuja oparesheni la ukaguzi wa vyombo vya moto”

Na,Daniel Manyanga

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu  kamishina msaidizi wa polisi ACP.Edith Swebe ametoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto mkoani hapo  kuhakikisha wanapeleka vyombo vyao vya moto kwenda kukaguliwa na jeshi la polisi ili kuepusha ajali ambazo siyo za lazima zinazotokea  kwa kusababishwa na ubovu wa vyombo wanavyovitumia.

Kamanda ACP, Edith Swebe  ametoa rai hiyo wakati akizungumza na madereva hao katika uzinduzi wa zoezi la ukaguzi wa vyombo vya moto mkoani Simiyu, uliofanyika  mjini Bariadi na kuwataka madereva hao kuhakikisha vyombo vyao vinakaguliwa.

Sauti ya RPC mkoa wa Simiyu ACP, Edith Swebe akitoa rai kwa madereva kuleta vyombo kukaguliwa

Kwa upande wake mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Simiyu SSP. Philbert Rwomunshaka  amesema kuwa zoezi limeanza toka Julai 16 na litaendelea kwa muda wa miezi mitatu.

Sauti ya RTO mkoa wa Simiyu akizungumzia oparesheni ya kukagua magari

Nao baadhi ya madereva wa vyombo vya moto mkoani Simiyu wakaomba jeshi la polisi liendelee kuwapa elimu ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

Sauti ya baadhi ya madereva wakiomba jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani