TRA yatoa elimu kwa wafanyabiashara ulipaji kodi kwa hiari
28 May 2024, 5:03 pm
Wafanyabiashara wilayani Maswa wamepewa elimu ya ulipaji kodi kwa hiari ili kujenga uchumi wa nchi, pia kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge na maafisa wa TRA kutoka wilayani hapo na mkoa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Simiyu imeendesha mafunzo kwa wafanyabiashara wilayani Maswa kuhusu elimu ya kulipa kodi kwa hiari ili kuleta huduma bora za jamii na uchumi wa taifa
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge amesema kuwa utunzaji wa kumbukumbu za mauzo ya bidhaa ni muhimu kwa mfanyabiashara pamoja na kuwa na uwazi na uzalendo katika kulipa kodi kwa hiari.
Mh Kaminyoge amesema kuwa lazima watoe rist za EFDs wanapofanya Manunuzi na Mauzo ya Bidhaa zao ili kuwarahisishia maafisa wa TRA kukadiria kodi kulingana na Mauzo yanayopatikana huku akiwataka wafanyabiashara ambao hawajafikia kuwa na EFDs watoe rist za Mkono ili kuweka kumbukumbu.
Meneja wa TRA Wilayani Maswa Lucius Theonesti amesema kuwa bado matumizi ya Mashine za EFDs ni madogo hivyo amewataka wafanyabiashara watumie hizo Mashine kwa walio na vigezo ili kuondoa malalamiko ya kukadiriwa Kodi kubwa.
Aidha amesititiza kwa Wafanyabiashara kuwa waaminifu na wazalendo kwani wapo baadhi yao wanapotembelewa na Maafisa wa TRA Wanaficha vielelezo vyao vya kumbukumbu ya Mauzo ili kukwepa kulipa Kodi halali.
Nao baadhi ya Wafanyabiashara John chagu na Zainabu Masoud wamesema ni vyema ikatumika Lugha ya Kiswahili katika Nyaraka za TRA ili kumrahisishia mteja kuelewa zaidi pamoja na kuwatembelea mara kwa Mara ili kuona changamoto zinazowakabiri ili kufanya Makadirio sahihi.