Pangani FM

Watu 900 watibiwa macho Pangani

20 September 2022, 2:53 pm

 

Zaidi ya watu 900 wamepatiwa matibabu ya macho katika Hospitai ya wilaya ya Pangani kati ya tarehe 10-15 mwezi huu.

Matibabu hayo yamefanyika kufuatia kambi maalum ya matibabu iliyowekwa Hospitalini hapo.

Pangani FM imezungumza na Dk. Joan Amos Kibula kutoka Hospitalini hiyo ambaye ameeleza kuwa kambi hiyo imefanyika kwa mafanikio na imewanufaisha pia wakazi wa wilaya jirani kama Lushoto, Muheza na Tanga.

Dk. Kibula amesema kuwa ingawa kambi hiyo maalumu ya matibabu  imefikia tamati Hospitali ya Pangani ina wataalamu wa macho hivyo Wananchi wanaendelea kupata matibabu, hivyo ameshauri watu kujiwekea utamaduni wa kwenda Hospitali na kuangalia Afya zao.

Zoezi hilo la utoaji wa huduma za matibabu ya macho bila malipo limefanyika kuanzia Septemba 10-15 Wilayani Pangani.