Chai FM

Maadili yatajwa kuwa mwarobaini wa vitendo vya ukatili

6 September 2023, 11:39 am

RUNGWE – MBEYA

Na Fadhili Mwaifulile

Jamii wilayani Rungwe Mkoani Mbeya imetakiwa kusimamia maadili kwa watoto wao hususani watoto wa shule za misingi na sekondari.

Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Rungwe ndg,ALLY KIUMWA kwenye sherehe za kufunga mafunzo kwa wahitimu ya wakulima wadogo wa chai Rungwe na busokelo yaliyofanyika kata ya masoko kwa amcos ya segela kwa jumla ya wahitimu 800, chini ya mradi wa Agricon boresha  chai .

Amesema kutokana na vitendo viovu vinavyo jitokeza kwenye  jamii kama vile ubakaji unapelekea mimba za utotoni kitendo kinacho katiza ndoto kwa watoto wa shule.

katibu tawala 1……………

Kwa mujibu wa KIUMWA amesema  kuwa mimba za utotoni ni changamoto kubwa huku akiwataka wazazi kuzungumza na watoto vizuri ili waweze kuepukana na changamoto hiyo inayo sababisha kukatiza ndoto zao mapema.

Aidha ametoa rai kwa vijana wote wanao warubuni watoto wa shule kuwa  serikali ipo macho na itafuatilia  kuwashungilikia watu wanamna hiyo wanao kwamisha ndoto za watoto wa kike.

 Katika hatua nyingine  amewakumbusha wananchi wote  kuimarisha afya zao ili kuondoa udumavu katika jamii zao

Katibu tawala lishe………………………….