Mila Kandamizi Zatajwa kuchangia Vifo vitokanavyo na Uzazi Wilayani Maswa..
29 October 2022, 6:23 pm
Imeelezwa kuwa Mila kandamizi kwa baadhi ya Jamii ikiwemo kabila la Wasukuma zinachangia vifo vitokanavyo na Uzazi kwa Wanaume Kushindwa kushiriki na Wenza wao kikamilifu katika Huduma ya Afya ya Uzazi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Kawiye Social Development Foundation- KASODEFO Marius Isavika wakati akitoa Elimu juu ya Mila Potofu zinavyochangia Vifo kwa akina Mama wajawazito kupitia Radio Sibuka fm.
Isavika amesema kuwa Jamii ya Wasukuma hasa kwa wanaume wamekuwa hawashiriki masuala ya Afya ya Uzazi ikiwemo kwenda kiliniki na mwenza wake nikujidhalilisha na kujishushia hadhi kwa mwanaume..
‘’Kwa sisi wasukuma kwenda na mke wako kiliniki nikujidhalilisha kwasababu Jamii itakuona umeshikwa na Mwanamke au kuonekana mwanaume Bwege Jambo ambalo siyo sahihi kwa Ulimwengu wa Sasa’’
‘’Ni vizuri Jamii yetu ikaelewa kuwa masuala ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango ni ya wote Baba na Mama kushirikiana pamoja kwa kwenda kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya na kukaa chini na kuamua muzae watoto wangapi na siyo jukumu la mama pekee yake’’
‘’Ninatoa wito kwa Wananchi hasa Wanaume Wilayani Maswa na Mkoa wa Simiyu kwa Ujumla kwasababu Sibuka fm inasikika sehemu Tofauti kubadilika na kuondoa Mila Potofu zinazochangia kwa sehemu kubwa vifo vya akina Mama Wajawazito’’
Elias John na Masanja Mabula ni Baadhi ya Wanaume waliozungumza na Sibuka Fm Radio wamekiri kutokushirikiana na Wenza wao katika Masuala ya Afya ya Uzazi kwakuwa Masuala ya Uzazi hayawahusu hivyo kuanzia sasa baada ya kupata Elimu hiyo watashiriki kikamilifu ili kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi..
‘’ Haya Masuala ya kusindikiza Wenza wetu kiliniki tulikuwa tunaona kuwa hayatuhusu sisi Wanaume , lakini kumbe yana Umuhimu sana katika kusaidia kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi kuanzia sasa hatutapuuza baada ya Elimu hii’’