UPATIKANAJI WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU YA MASUALA YA AFYA YA UZAZI VYATAJWA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI WILAYANI BUSEGA MKOANI SIMIYU.
27 April 2022, 9:15 am
Imeelezwa kuwa Wilaya ya Busega iliyopo Mkoani Simiyu imepunguza kwa kiasi kikubwa Vifo vitokanavyo na Uzazi kutokana na Upatikanaji wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya na Elimu ambayo imekuwa ikitolewa kupitia njia mbalimbali ikiwemo Radio Sibuka Fm.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Mh, Gabriel Zacharia Wakati akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu Hasani Madarakani mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama na Wadau mbali mbali wa Maendeleo wilayani hapo.
Insert 01. David Zacharia
Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Zaidi ya Shilingi Bilioni mbili zimeletwa katika Wilaya ya Busega kwa Ajili ya kutatua changamoto ya Huduma za Afya ikiwemo Ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati, Ukarabati na Ukamilishaji Maboma yaliyokuwa yameanzishwa..
Inser 02. David Zacharia
Mh Zacharia amesema Pamoja na kufanya vizuri katika Sekta ya Afya bado kuna changamoto ya Wilaya kuongoza kwa Watoto wa kike kukatizwa ndoto kwa kupewa Ujauzito na kuwata wadau kushirikiana kuwafichua wanaume ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo vya kikatii ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria ..
Insert 03. David Zacharia.