Vifo vitokanavyo na Uzazi vyapungua Wilayani Maswa
19 April 2021, 5:09 pm
Vifo vitokanavyo na Uzazi wilayani Maswa mkoani Simiyu vimepungua kutoka vifo 12 kwa mwaka 2018 hadi kufikia vifo 3 kwa mwaka 2020.
Takwimu hizo zimetolewa na Mratibu wa Huduma ya Mama ya mtoto kutoka Hospitali ya wilaya ya Maswa Angella Ngaiza wakati akitoa Elimu ya Afya ya Uzazi kupitia Radio Sibuka fm.
Bi Ngaiza amesema kuwa kupungua kwa vifo hivyo kumetokana na Mikakati ya Halmashauri ya wilaya, Wadau wa Afya na kituo cha Radio Sibuka kwa kusaidia kutoa Elimu ya Afya ya Uzazi na kuwafika watu wengi zaidi na kuongeza kuwa vifo hivyo vinapoteza nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Mratibu huyo wa Huduma ya Mama na Mtoto amesema kuwa Ushiriki wa Mwanaume katika Huduma ya Afya ya mama kuna nafasi kubwa ya Mama kujifungua Salama Hivyo ni vyema Jamii ikaondoa mazoea na dhana ya kuwa wazazi wa zamani walikuwa wanajifungulia nyumbani bila madhara yoyote kwani kwa sasa mambo yamebadilika.