Sibuka FM

RC Macha amaliza mgogoro wa fidia kwa wananchi

17 March 2026, 1:22 pm

Pichani aliyevaa mkoti wa dark blue na miwani ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, kulia kwake aliyevaa kaunda suti za blue ni mkuu wa wilaya ya Maswa,Dkt.Vicent Naano Anney wakiwa katika moja wapo ya shughuli za kiserikali Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Ni kweli hakuna mtu asiyependa maendeleo ya nchi yake kila wananchi anatamani kuona miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wingi bila changamoto zozote zile za kimaslahi kwa wale wanaopaswa kulipwa fidia zao kutokana na kupisha miradi hiyo katika maeneo hayo”.

Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha amesema kuwa serikali ya mkoa huo itaendelea kusimamia na kuhakikisha wananchi wake wanapata haki sawa kwenye maeneo yao yanayochukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuondoa migogoro ya ardhi hasa kwa wamiliki wa maeneo hayo.

Anamringi Macha  ameyasema hayo wakati akipokea ripoti ya uthamini ardhi wa mara ya pili uliofanyika kwa ajili ya kutatua mgogoro wa fidia uliokuwepo kati ya chuo cha usimamizi wa fedha na mipango (IFM) kampasi ya Simiyu, na wananchi wa kijiji cha Sapiwi ambao walikuwa wamegomea fidia ya awali wakidai kuwa ilikuwa haiendani na thamani ya ardhi iliyochukuliwa na chuo hicho kwa ajili ya ujenzi wa chuo.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha

Silas Honga ni mthamini mwandamizi wa ardhi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya utatuzi wa mgogoro huo ameeleza matokeo ya uthamini huo wa mara ya pili huku mkuu wa idara ya mipango na maendeleo wa chuo hicho Dkt. Ezra Kakozi akisema kuwa fedha hizo zitalipwa kwa wahusika kwa wakati mwafaka.

Sauti ya Silas Honga na Dkt.Ezra Kakozi

Songolo Mayuma, Suleiman Mayongela na Emmanuel Maseko  ni baadhi ya wananchi waliokuwa wamegomea fidia ya awali wamesema kuwa wamekubaliana na uthamini huo wa mara ya pili na kwamba wako tayari kupokea fidia itakayotolewa kwa sasa.

Sauti ya wananchi