Sibuka FM

Wakulima wa pamba waomba sheria kali waliochezea mizani msimu mwaka jana Simiyu

6 March 2026, 9:27 am

Pichani aliyevaa suti ya dark bluu mwenye miwani ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Vicent Naano Anney pamoja na viongozi wengine wakipatia maelekezo wakati wa mkutano mkuu wa 8 wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Simiyu SIMCU Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Tunatumia nguvu kazi kubwa sana hadi pamba kufika sokoni tukitarajia tutapata faida kutokana na kile ambacho tumekifanya kwa msimu mzima wa kilimo halafu panatokea mtu mmoja tu anaanza kutengeneza faida kutokana na jasho la watu wengine hii haipo sawa tunawavunja moyo wakulima wetu”.

Na,Daniel Manyanga 

Wakulima wa zao la pamba mkoani Simiyu wameiomba serikali ya mkoa kuwashughulikia wanunuzi wa pamba waliofanya udanganyifu msimu wa mwaka jana wa kuwaibia wakulima wakati wa mauzo kg 20 kwenye kila kg 100 baada wa wanunuzi hao kuchezea mizani.

Julai mwaka jana wakala wa vipimo mkoani hapa walifanya oparesheni ya kushtukiza na kubaini uwepo wa mizani iliyochezewa  na baadhi ya watu waliokutwa walikimbia  na katika oparesheni hiyo jumla ya mizani 180 ilikaguliwa na 60 ilikutwa imechezewa na kufatia sakata hilo la baadhi ya wahusika kujulikana  na hatua kali za kisheria zimeanza kutekelezwa kwa wale wote waliohusika kuwaibia wakulima wa zao la pamba.

Wakizungumza na SibukaFm,George Heke,Emmanuel Myembela na Paulo Makalanga ambao ni wakulima wa pamba kupitia viongozi wao  wameiomba serikali kuwachukulia hatua wahusika wote ili iwe fundisho kwa wanaotaka kuendelea na mchezo huo kabla ya msimu mpya wa manunuzi kuanza ili kuleta tija kwa wakulima hao kutokana na kazi ngumu wanayoifanya ya kilimo hicho.

Sauti ya wakulima wa zao la pamba wakiomba sheria kali kwa wezi wa zao hilo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha amesema msimu uliopitia jambo lililowasumbua wakulima wa pamba mkoani hapa baada ya msimu wa uuzaji wa pamba kufunguliwa ni baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu  kuchezea mizani  hali iliyopelekea kutofikia matarajio ya mauzo waliyoyakusudia hivyo msimu huu haitatokea na lazima sheria kali zichukuliwe kwa wale wote waliobainika kufanya mchezo huo mchafu kwa wakulima wa pamba.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akielezea hatua zitakazochukuliwa kwa waliobainika kuwaibia wakulima