Sibuka FM
Sibuka FM
5 February 2026, 8:18 pm

“Maendeleo bila watu hayo siyo maendeleo katika kujenga nchi yetu lazima kwanza tuhakikishe usalama wa wananchi maana hawa ndiyo walipa kodi za maendeleo ya taifa ukiona nchi inauchumi imara nyuma yake kuna watu na siyo wanyama”.
Na,Daniel Manyanga
Mtoto mmoja kati ya watatu waliokuwa wakioga kwenye mto Simiyu uliopo kata ya Zanzui wilayani Maswa mkoani Simiyu ameuwawa na mamba huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimeliwa ikiwemo mguu,viungo vya ndani ya tumbo na sehemu ya makalio ikiwa imeliwa na mnyama huyo.
Wakizungumza na Sibuka Fm baadhi ya wanakijiji wamemtambua mtoto huyo kwa majina ya Paulo Petro Bunga mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa wa pili kutoka kwenye maji lakini mamba akampiga na mkia na kumzamisha kwenye maji huku wenzake wawili wakishuhudia tukio hilo mmoja aitwaye Baraka akiwa ndani ya maji na Emmanuel Robert akiwa yupo nje ya maji baada ya kuwa wa kwanza kutoka.
Emmanuel Robert ni mmoja wa wanusura ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Zanzui iliyopo wilayani hapa anaeleza tukio lilivyokuwa.
Mussa Maige ni mkazi wa kijiji cha Malita amesema kuwa mwili wa mtoto huyo umekutwa ukiwa hauna mguu mmoja,viungo vya ndani ya tumbo vimeliwa,sehemu za siri na makalio pia yameliwa.
Wakizungumza kwa simanzi kubwa baadhi ya wananchi wa maeneo hayo,Mussa Maige,Ng’abhi Konza na Florencia Jingila wakaiomba serikali iwatege mamba hao kutokana na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kutegemea maji ya mto huo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo pamoja na kuwachimbia visima virefu ili kupekana na adha hiyo kutokana na matukio hayo kujirudia mara kwa mara.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Miza Jishuli na Katibu wa CCM wilaya hiyo ,Ephraim Kolimba wameomba kwa mamlaka husika za wanyama kusakwa kwa mamba huyo.