Sibuka FM

Ofisi ya DC Maswa yaunda kamati ya kusikiliza  migogoro ya wananchi

3 February 2026, 9:09 am

Picha : aliyeshika mic ni Mhe Enos Missana Hakimu mfawidhi mahakama ya wilaya ya Maswa wakati wa sherehe ya siku ya sheria nchini

Utawala wa sheria ndio nguzo muhimu katika kuleta Ustawi na  Maendeleo kwa Nchi, hivyo Mahakama ina mchango mkubwa ” Enos Missana

Ofisi ya  Mkuu  wa  Wilaya ya Maswa, Mkoani  Simiyu  imeunda  kamati  maalumu  kwa ajili ya kusikiliza na kutatua  kero na  Migogoro mbalimbali ili kusaidia wananchi  kupata  haki zao  za msingi kwa  urahisi  ambapo kila  Alhamisi ya wiki imekuwa  ikisikiliza migogoro na  malalamiko ya wananchi

Akizungumza  katika Sherehe ya  siku ya  Sheria  Nchini, Katibu tawala  Wilaya ya Maswa  ndugu  Athuman Kalaghe   akimuwakilisha   Mkuu wa  Wilaya  hiyo  Dkt  Vicent Naano Anney   amesema  kuwa kuanzishwa kwa  kamati hiyo kutasaidia kuleta  ustawi kwa  Wananchi  huku  akitoa  pongezi  nyingi kwa  Mahakama za Maswa  kwa kusimamia Haki  vizuri hali inayofanya malalamiko ya wananchi kupungua

sauti ya Athuman Kalaghe -DAS Maswa akizungumza wakati wa siku ya sheria nchini

Kwa  upande  wake  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi   Mkahakama ya wilaya ya Maswa   Mhe  Enos  Missana  ambae  alikuwa  Mgeni  rasmi  katika  sherehi hiyo  amesema  kuwa  utawala  bora  ndio  nguzo  muhimu katika  kuleta  Ustawi na  Maendeleo  kwa  Nchi  kwani   Mahakama  ndio  chombo kinachotofasri  sheria, kulinda  haki za  binadamu  na kuhakikisha  hamna  mtu  aliye juu ya  sheria

sauti ya Enos Missana Hakimu mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Maswa

Aidha  Mhe  Missana  ametoa  wito  wa  wadau  wa  sheria  kushirikiana na  mahakama ili  kufikia  malengo endelevu  na  ustawi  wa  Taifa  hivyo  bila  kuwa   sheria  bora  hakuna utaratibu  bora  wa  kijamii

sauti ya Enos Missana Hakimu mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Maswa
Mhe Suzan Masule- mwendesha mashtaka -NPS

Suzan  Masule ni  mwendesha mashtaka kutoka Ofisi ya  Taifa ya mashtaka  wilaya ya Maswa  amesema kuwa  ili mahaama  iweze kutoa  mchango katika ustawi  na Maendeleo ya  Nchini ni lazima mahakama iwe  huru kutoka kwenye ushawishi , Msukumo au vitisho kutoka  muhimili mwingine

sauti ya Suzan Masule akizungumza wakati wa sherehe ya siku ya Sheria nchini

Naye Daudi Masunga  kutoka  Chama cha Wanasheria  Tanganyika  – TLS   amesema  kuwa  wataendelea  kutoa  ushauri  wa  kitaaluma kwenye mabadiliko na  marekebisho  ya sheria  mbalimbali huku akiipongeza  mahakama  kwa  maboresho ya  makubwa ya  mifumo ya uendeshaji  wa  mashauri kupitia mfumo wa Tehama

sauti ya Daudi Masunga kutoka TLS akizungumza wakati wa siku ya sheria nchini

pichani ni baadhi watumishi wa Mahakama wakisikiliza ujumbe wa siku ya sheria nchini
picha ni baadhi ya wananchi waliohudhuri siku ya sheria nchini katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Maswa