Sibuka FM

Kilimo cha umwagiliaji mkombozi mwenye tija Simiyu

12 January 2026, 3:36 pm

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde akizungumza jambo na wananchi hawapo pichani baada ya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa katika kata ya Kasoli Picha kutoka Maktaba ya Sibuka FM

Haiwezekani kila kukicha wakandarasi wazama kuilalamikia serikali kutowapatia miradi na badala yake wanawapatia tu wageni swali tu dogo ni lini wakandarasi hao wameomba na hawakupata je vigezo wanatimiza na wanatekeleza kwa ubora bila ya kuwa chenga chenga.”

Na,Daniel Manyanga 

Naibu waziri wa kilimo David Silinde amewataka wakandarasi wazawa wote wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji nchini kuhakikisha wanakuwa waaminifu na watekeleze miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa ili kuongeza imani kubwa waliyopewa na serikali katika jukumu hilo la kuwahudumia wananchi katika kuongeza tija ya kilimo.

Naibu waziri ,Silinde ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya aujenzi wa bwawa la umwagiliaji unaoendelea katika kata ya Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu, baada ya diwani wa kata hiyo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi ,Mayala Lucas kuhoji mkandarasi aliyekuwa anachimba mifereji ya umwagiliaji kuondoka eneo la mradi kabla ya kukamilisha kazi.

Sauti ya mwenyekiti na naibu waziri wa kilimo

Kwa upande wao wananchi na mwenyekiti wa halmashauri ya Bariadi DC wakaeleza matarajio yao pindi mradi huo utakapokamilika na kuanza kutumika.

Sauti ya wananchi wakielezea faida watakazopata kama mradi huo utakamilika

Katika hatua nyingine naibu waziri,David Silinde amewaomba wananchi kuiunga mkono miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao na siyo kuwa sehemu ya kukwamisha miradi hiyo ya maendeleo.

Sauti ya naibu waziri wa kilimo David Silinde akizungumza na wananchi na kuwaelezea faida ya mabwawa hayo