Sibuka FM

Jela miezi 9 kwa kuua kwa maneno baba yake Itilima

18 December 2025, 12:34 pm

Pichani ni muonekano wa nje wa jengo la mahakama ya wilaya ya Itilima ilipofanyika hukumu ya ,Dunili Mageme ya kwenda jela miezi tisa baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuua kwa maneno baba yake mzazi Picha kutoka

Vijana vijana vijana nawaita mara tatu tafuteni mali zenu za halali kwa kutoa nguvu, akili, uwezo uliopewa na Mungu achaneni kuanza kutamani urithi angali wazazi wako bado wapo hai hapo ni kuliaibisha kundi la vijana taifa la leo na kesho fanya kazi acha uzembe wa kufikiri”.

Na, Daniel Manyanga

Mahakama ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu amemhukumu mtu mmoja kwenda jela miezi tisa kwa kosa la kutishia kumuua baba yake mzazi huku kisa kikitajwa kuwa kutaka kuuza maeneo ya baba yake mzazi bila ruhusa ya mmiliki wa maeneo hao.

Aliyehukumiwa ni Dunili  Mageme mwenye umri wa miaka 56 mkazi wa kijiji cha Mwamugesha na ameshtakiwa katika  mahakama ya wilaya ya Itilima  kwa kosa moja la kutishia kuua kwa maneno  kinyume na kifungu cha 89(2) (a) na (b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2023 .

Awali mahakamani hapo imedaiwa na mwendesha  mashtaka mkaguzi wa jeshi la polisi, Jaston Mhule  kuwa mnamo Oktoba 15, 2025 katika kijiji cha Mwamugesha  ndani ya wilaya ya Itilima mhanga mwenye umri wa miaka 90 alitishiwa kuuawa na kijana wake na taarifa zilifika kwenye ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Mwamugesha na baadae kituo cha polisi  Itilima  ambapo mshtakiwa alikamatwa  na  kufikishwa kituo cha polisi Itilima  kwa mahojiano zaidi ya kujuwa nini shida ya kutaka kumkatisha uhai baba yake mzazi na  baada ya upelelezi kukamilika mnamo Oktoba 22,2025 alifikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Hukumu hiyo shauri la jinai kesi Na.25673/2025 iliyosomwa mbele ya hakimu  mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Itilima,Mhe.Robert Kaanwa huku upande wa mashtaka wakileta  jumla ya mashahidi wanne 04 na mshtakiwa akijitetea mwenyewe akiwa na mashahidi watatu na ndipo mahakama ya wilaya ya Itilima ilimtia hatiani mshitakiwa pasina kuacha shaka yoyote kwa pande zote mbili.

Baada ya kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo mshitakiwa apewe adhabu kali ili iwe funzo kwake na kwa jamii kwani tukio hilo  nikujichukulia sheria mkononi  na matukio ya mtindo huu yamekua yakipelekea matukio ya mauaji  na wahanga wakubwa ni  kundi la wazee ambapo wengi wao wakati mwingine wanahusishwa na mambo ya kishirikina.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani anafamilia ina mtegemea na mara yake ya kwanza kutenda kosa la bila kukusudia licha ya kutamani mali za mzee wake ndipo hakimu  mkazi mwandamizi wa wilaya ya Itilima ,Mhe.Robert Kaanwa alimhukumu kwenda jela  miezi 09 kwa kosa kujaribu kuua kwa maneno bila kukusudia

Mara baada ya hukumu hiyo kusomwa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Itilima, Mhe.Robert Kaanwa baba mzazi wa mshitakiwa akaipongeza mahakama kwa kutenda haki kwa upande wake kwani vitendo vya kijana wake vimekuwa vya muda mrefu sana kumtishia kumuua kila urithi.

Sauti ya baba mzazi wa mshitakiwa, Dunili Mageme akiishukuru mahakama hiyo kutenda haki bila upendeleo