Sibuka FM
Sibuka FM
24 November 2025, 11:41 am

Mahitaji ya damu katika Hospitali ya wilaya yetu ni makubwa ukilinganisha na upatikanaji wake, hivyo natoa wito kwa jamii kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu. ” Peter Shimba Mratibu wa damu salama hospitali ya wilaya ya Maswa “
Wananchi Wilayani Maswa, mkoani Simiyu wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la uchangiaji wa Damu ili kuokoa maisha ya watu wengine wenye uhitaji wa Damu, ambapo zoezi hilo likiratibiwa na Kituo cha Afya cha Barikiwa kilichopo maswa mjini maeneo ya mnadani.
Wakizungumza na Sibuka fm baada ya kuchangia damu, wananchi hao wamesema kuwa zoezi ni zuri hivyo wananchi wengine wajitokeze kuchangia damu pamoja upimaji wa magonjwa mbalimbali yakiwepo magonjwa yasiyo yakuambukizwa

Dr Ashley Lucas ni Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Barikiwa amesema kuwa wameamua kuja na kampeni hiyo lengo ni kusogeza huduma za afya kwa jamii na kutambua hali zao za kiafya kwa kupima bila gharama yoyote hivyo wananchi wajitokeze
Kwa upande wake mratibu wa Damu salama kutoka Hospitali ya wilaya ya Maswa Dr Peter Emmanuel Shimba amesema mahitaji ya damu ni makubwa ukilinganisha na upatikanaji wake hasa wakati ambao shule zikiwa zimefungwa hivyo jamii iguswe kuchangia huduma hiyo ya damu
Aidha Dr Shimba ametoa wito kwa jamii kujitokeza kuchangia damu kwa mahitaji ni makubwa hasa watoto wenye seli mundu, akina mama wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na watu wanaopata ajali huku akiwashuru wadau wa Kituo cha Afya cha Barikiwa kwa kutoa sapoti pamoja na kuratibu zoezi hili muhimu linalolenga kuokoa maisha ya Watanzania

Katika kampeni hiyo iliyoambatana na mashindano ya fainali ya mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na kituo hicho cha Barikiwa, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt Vicent Naano Anney akatoa wito kwa Jamii kuwa na tabia ya kupima afya huku akaahidi kuanzisha ligi nyingine ndogo ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 9 Disemba siku ya Uhuru wa Tanganyika

