Sibuka FM
Sibuka FM
23 November 2025, 3:07 pm

Serikali Mkoa wa Simiyu inatarajia kutoa Hati za kimila 6000 kwa wakulima na wafugaji kutoka Halmashauri sita za mkoa ili kuongeza thamani ya maeneo yao na kuchochea utunzaji wa mazingira kupitia mradi wa mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza na waandishi na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji, Meneja mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mkoa wa Simiyu Mhandisi Gogadi Mgwatu amesema kuwa mradi huo unakusudia kurejesha uoto wa asili kwa kupanda miti na nyasi za malisho.

Mhandisi Kahabi Medard ni afisa kutoka mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi anaeleza maeneo matatu ambayo mradi umejikita huku akitaja manufaa yatakayopatikana kutokana na mradi huo ambao upo chini ya Wizara ya maji.
Kwa upande wake Raymond Makanga kutoka Simiyu Climate Resilience Project- SCRP amesema kuwa wametoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji zaidi ya 200 kutoka Halmashauri Sita za mkoa wa Simiyu ili kwenda kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kurejesha uoto wa asili
Nao baadhi ya wakulima na wafugaji walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia suluhu Hasan kwa mradi huo utaoenda kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji kwani maeneo yatapimwa na kupatiwa Hati pamoja kupanda miti ya marisho kwa wafugaji


