Sibuka FM
Sibuka FM
21 November 2025, 12:45 pm

“Amani ya nchi ndiyo msingi wa maendeleo katika taifa lolote lile amani ikikosekana hapo maendeleo hakuna maana hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kufanya shughuli za uchumi muda huo anawaza kukimbia machafuko mfano mzuri tu angalia miji kama Goma,Kivu ni miji iliyojaa utajiri wa madini lakini watu wake ni masikini wa kutupwa”.
Na,Daniel Manyanga
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Bariadi mkoani Simiyu, ASP Yusuph Abdallah amewataka maafisa usafirishaji wa bajaji na bodaboda kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu vinavyovunja amani ya nchi.
Akizungumza na maafisa usafirishaji hao kwenye kikao cha pamoja kilichowakutanisha waendesha bodaboda na bajaji mjini Bariadi,ASP Yusuph Abdallah amewaomba maafisa hao kuacha mara moja kujihusisha na vitendo hivyo badala yake wawe mabalozi wazuri wa kuihubiri amani ya nchi hii.
ASP,Abdallah ameongeza kuwa vitendo vya kujihusisha na maandamano yasiyokuwa na kibari cha jeshi la polisi ni kosa la uhalifu hivyo unaweza kukutana mkono wa sheria kali kwa mjibu wa katiba ya nchi hii.
Paul Mboyi ni mmoja wa maafisa usafirishaji aliyeshiriki kikao hicho amewaomba waendesha bajaji na Bodaboda kuwa mstari mbele katika kulinda amani ya nchi na kuacha kushiriki vitendo vya uvunjifu wa amani ambapo ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.
Wakizungumza kwenye kikao hicho ,Samwel Chacha katibu wa waendesha bajaji mkoa wa Simiyu na Abel Magembe mwenyekiti wa waendesha Bodaboda mkoa wa Simiyu wamesema kuwa amani ya nchi ikipotea hakuna maendeleo hivyo ni vyema kuilinda tunu iliyoachwa na muasisi wa taifa hili Mwl.Julius Kambarage Nyerere.