Sibuka FM
Sibuka FM
28 October 2025, 11:35 am

Nimezunguka kata zote 19 za Jimbo la Maswa mashariki nimesikiliza kero na kujionea changamoto mbalimbali hivyo mkinipa ridhaa ya kuwa mbunge wenu nitaenda kuzitatua ” Dkt George Lugomela”
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Mashariki Mkoani Simiyu kupitia chama cha mapinduzi –ccm Dkt George Venance Lugomela amehitimisha kampeni zake za uchaguzi kwa kishindo baada ya kuzunguka kata zote kumi na tisa na kusikiliza kero na changamoto za wananchi wa jimbo hilo.
Katika ahadi zake Dkt Lugomela amesema kuwa endapo wananchi wa Maswa watampa ridhaa ya kwenda kuwawakilisha huko Bungeni atahakikisha suala la maji anaanza nalo kwani ndio changamoto kubwa kwa wananchi wa Maswa pamoja na sekta nyingine nyingine za Afya, Elimu, Kilimo, Mifugo na Miundombinu
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Ndugu Shemsa Mohamed amewaomba wana Maswa wakichague chama cha Mapinduzi kuanzia nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani kwani ndio chama pekee kinachowaletea maendeleo wananchi hivyo ni vyema uweka mafiga matatu.

Stanslaus Nyongo ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi – NEC na mbunge mstaafu wa Jimbo la Maswa mashariki amesema kuwa Mhe Dkt Rais Samia Hasani amefanya mambo makubwa ya maendeleo katika wilaya ya Maswa hivyo wana maswa wakampe kura nyingi za kutosha ili aendelee kuleta fedha za maendeleo

