Sibuka FM

Makundi maalumu kupewa kipaumbele Uchaguzi mkuu

26 October 2025, 3:30 pm

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Maswa mashariki na Maswa Magharibi Ndugu Julius Ikongora John akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura. Picha na Nicholaus Machunda

Siku ya uchaguzi tarehe 29 mwezi Oktoba 2025, nawasihi wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo mkatoe vipaumbele kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha “Julius Ikongora John Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Maswa”

Na Mwandishi wetu

Msimamizi  wa Uchaguzi  Jimbo la Maswa Mashariki na Maswa Magharibi  Mkoani Simiyu amewataka wasimamizi wa Uchaguzi  kwenye  vituo vya kupigia kura kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa  makundi maalumu ya Wazee, Wajawazito, watu wenye Ulemavu na  akina mama wanaonyonyesha

Hayo ameyasema  leo  Oktoba  26, 2025  wakati wa  ufunguzi  wa  mafunzo kwa  Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa  vituo vya  kupigia kura  na kuwataka wazingatia  makundi  hayo  ili kuepuka  usumbufu kwenye  vituo vya  kupigia  kura

Sauti ya Julius Ikongora John akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uchaguzi

Ikongora  ameongeza  kuwa  wasimamizi hayo wa  vituo vya  upigia  kura wanapaswa  kutunza  siri za  tumekulingana  na  kanuni za Tume huru ya Taifa  ya uchaguzi  hivyo kukiuka  viapo kunaweza kuwatia  hatia   kwa  mjibu wa  sheria, miongozo  na  katiba  ya Tume

Sauti ya Julius John akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uchaguzi

Nao wasimamizi na  wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya  kupigia  kura  wanaeleza namna walivyopokea mafunzo na  kuahidi kutekeleza  majukumu yao  kwa  mujibu wa  sheria, Kanuni na Miongozo ya Tume huku wakitoa kipaumbele  kwa  makundi maalumu, wananchi wajjitokeze  kwa  wingi siku ya  uchaguzi wa Rais, Wabunge  na Madiwani  ifikapo Oktoba 29, 2025

Sauti za washiriki wa mafunzo ya uchaguzi wakielezea walivyojiandaa na zoezi la uchaguzi

Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika tarehe 29, Oktoba, 2025 ambapo katika Jimbo la Maswa mashariki na Jimbo la Maswa magharibi, Jumla ya wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya upigia kura 2043 wamepewa mafunzo kwa ajili ya usimamizi wa zoezi hilo.

Picha za matukio mbalimbali ya mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura