Sibuka FM
Sibuka FM
22 October 2025, 2:46 pm

“Kuchagua kiongozi unayemtaka ni takwa la kikatiba katika kuleta maendeleo kwenye eneo husika ndiyo maana sasa unapofika uchaguzi tunawataka wananchi waweze kuitumia hiyo haki ya kuchagua kiongozi wamtakao wenyewe”.
Na,Daniel Manyanga
Wilayani Maswa mkoani Simiyu imeelezwa kuwa wale wote waliopoteza kadi ya kupigia kura watatumia Leseni ya udereva,Kitambulisho cha Taifa(NIDA) na hati ya kusafiria(Paspoti) wakati wa kupiga kura siku ya uchaguzi ili nao waweze kutimiza takwa la kikatiba la kumchagua kiongozi kwa ngazi ya Udiwani,Ubunge na Urais mnamo tarehe 29.10.2025.
Akizungumza na Sibuka Fm msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Maswa Mashariki na Maswa Magharibi wilayani hapo,Julius John ametaja vitu vya kuzingatia kwa wale ambao wamepoteza kadi ya kupigia kura siku hiyo ya uchaguzi.
Julius ameongeza kuwa vituo vitakavyotumika kupigia kura ni vile vilivyotumika wakati wa zoezi la kujiandisha katika daftari la kudumu la wapiga.
Katika hatua nyingine msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Maswa Mashariki na Maswa Magharibi,Julius John amewaomba Wananchi kuhakiki majina yao katika vituo walivyojiandikishia kabla ya siku ya uchaguzi.