Sibuka FM
Sibuka FM
22 October 2025, 12:29 pm

Wazee ni hazina ya Taifa maana wamelitumikia kwa nguvu zao zote hivyo tunapaswa kuwajali na kuwatunza ili wasiwe omba omba na kunyanyasika– ” Georges Busungu -Mgombea Urais Ada tadea “
Mgombea Urais kupitia Chama cha African Democratic Alliance Party ( ADA – TADEA) Mhe Geoerges Busungu amesema kuwa endapo wananchi watakipa ridha chama hicho kuongoza Nchi kitahakikisha wazee wote wanalipwa Posho ya kujikimu ili kuepusha tatizo la kuwa Omba omba
Mhe Busungu amesema hayo wakati wa Mkutano wa kampeni za kunadi Ilani ya chama hicho ulifanyika katika kata ya Malampaka wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu na kusisitiza kuwa wazee ndio hazina ya Taifa hivyo ni muhimu kuwajali
Mgombea Urais huyo ameongeza kuwa Tanzania inaweza kubadilika iwapo wananchi tutaamua kubadilisha fikra zetu ili kuleta mapinduzi ya Kiuchumi ambapo makundi ya Wakulima, wafugaji, Wafanyakazi na wafanyabiashara yatahusishwa kikamilifu

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Salehe Mohamedi Msumari amesema kuwa endapo wananchi watakiweka madarakani kipaumbele kitakuwa Afya bure, Elimu bure hadi chuo kikuu na siyo kama ilivyokwasasa afya bure lakini watu wanaendelea kuchajiwa fedha za matibabu
Charles Mwinuka ni Mgombea Udiwani kata ya Malampaka kupitia Chama cha Ada Tadea amewahakikishia maendeleo katika Mji huo endapo watamchagua kuwa mwakilishi wao kwa ngazi ya kata hivyo wawe na imani nae.


