Sibuka FM
Sibuka FM
8 October 2025, 8:48 am

Niwapongeze sana Hospitali ya Barikiwa kwa kutekeleza azima ya Serikali ya kusogeza huduma kwa wananchi hivyo niwasihi wananchi wa Maswa na viunga vyake waitumie vyema fulsa hii ya Ujio wa Kambi ya Madaktari Bingwa ” Dkt Vicent Naano Anney Mkuu wa Wilaya ya Maswa “
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney amewataka Wananchi kutumia fulsa ya ujio wa madaktari bingwa katika Hospitali ya Barikiwa iliyopo wilayani hapo ili kupata matibabu ya magonjwa mbalimbali.
Mhe Dkt Anney ametoa wito huo baada ya Madaktari bingwa hao kuripoti ofisini kwake wakitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila kwa ajili ya kuja kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Wilaya ya Maswa na Wilaya jirani za mkoa wa simiyu
Aidha Mkuu wa Wilaya ameipongeza Hospitali ya Barikiwa kwa Ubunifu waliofanya wa kuleta huduma za Madaktari bingwa ili kusogeza huduma kwa Wananchi na kupunguza gharama za matibabu ambazo wangezipata katika Hospitali kubwa za rufaa na Kanda

Dr Hildegard Ashley Lucas ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Barikiwa amesema kuwa lengo la kuleta madaktari bingwa hao ni kusogeza huduma kwa wananchi na kusaidia upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa gharama nafuu na zenye ubora zaidi huku Bima mbalimbali za afya zikipokelewa
Nao baadhi ya madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila wamesema kuwa wapo Maswa katika Hospitali ya Barikiwa kwa Kambi Maalumu ya Magonjwa ya mfumo wa ndani, wagonjwa ya akina mama, mfumo wa Uzazi , kinywa na Meno, Upasuaji na mifupa hivyo wananchi wajitokeze kupata vipimo na matibabu bora

