Sibuka FM
Sibuka FM
7 October 2025, 2:02 pm

“Duniani hapa watu ni wengi lakini binadamu ni wachache na ukishangaa ya hapa duniani basi unabidi pia ushangae ya Mussa Shija na Hollo Shija kuoana hali ya kwamba ni kaka na dada tena mama mmoja na baba mmoja sasa hapa ndiyo kusema walikuwa hawajuani au ndiyo kusema funika kombe wanaharamu apite lakini je sheria walikuwa hawajui kuwa zipo kwa ajili ya wahalifu”.
Na,Daniel Manyanga
Mahakama ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imewahukumu Mussa Shija miaka 32 na Hollo Shija miaka 36 wasukuma na wakulima ambao ni kaka na dada wa damu kwenda jela miaka 20 na 30 kuoana (kuzini na maharimu ) katika kesi ya jinai shauri namba 10745/2025 iliyosomwa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe.Azizi Khamis.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Maswa Mhe.Aziz Khamis mwendesha mashtaka wa serikali mkaguzi wa polisi ,Vedastus Wajanga amesema kuwa washtakiwa wote wawili walishtakiwa kwa kosa la kuzini na maharimu kwa maana ya kujamiana na ndugu yako wa damu ambapo ni kinyume na kifungu cha 158(1) (b) na kifungu cha 160 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.
Awali mahakamani hapo ilidaiwa na upande wa jamhuri kuwa mnamo tarehe na miezi tofauti mwaka 2018 hadi tarehe 30 July 2024 katika kijiji cha Mandang’ombe washtakiwa wote wawili wakiwa ni ndugu wa damu kwa maana watoto wa baba mmoja na mama mmoja walijamiana na kuishi kama mke na mme na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume.
Mwendesha mashtaka huyo ameendelea kuiambia mahakama kuwa mnamo tarehe 31/07/2024 washtakiwa wote wawili walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Maswa na walipohojiwa walikubali kutenda kosa hilo kisha walifikishwa mahakamani tarehe 12/08/2024 na kusomewa makosa yao na walihukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa mshatakiwa, Mussa Shija na Hollo Shija alihukumiwa kwenda jela miaka 30.
Washtakiwa wote wawili walikata rufaa mahakama kuu na mahakama kuu ikaamru shauri lisikilizwe upya katika mahakama ya awali iliowahukumu ambapo mnamo tarehe 06/05/2025 washtakiwa wote wawili walifikishwa mbele ya mahakama tena na walisomewa mashtaka yao ambayo ni kuzini na maharimu na kisha walikana kutenda makosa hayo.
Upande wa Jamhuri ulileta jumla ya mashahidi kumi na moja na vielelezo vitano vilitolewa ikiwemo taarifa DNA ya uchunguzi wa kisayansi kutoka ofisi ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali ambayo ilithibisha kuwa asilimia 99.99% Mussa Shija na Hollo Shija ni watoto halali wa Shija Kamuga ambae ndie baba yao mzazi na asilimia 99.9% mtoto waliozaa washtakiwa pindi wanaishi kama mke na mme ni mtoto wao halali.
Watuhumiwa walipopewa nafasi yakujitetea mahakamani hapo mshtakiwa wa kwanza ,Mussa Shija alidai kuwa yeye ni yatima kwa maana hana baba wala mama na wazazi wake wamefariki nakumuacha akiwa mtoto mdogo nakulelewa na bibi yake mzaa mama na Hollo Shija ni mke wake halali ambae amemtolea mahali laki tatu na ishirini natano elfu na alimpa bibi yake na ,Hollo Shija mzaa mama na mshtakiwa wa pili nae alidai kuwa na yeye ni yatima na wazazi wake wamefariki akiwa mdogo na amelelewa na bibi yake mzaa mama pia Shija Kamuga siyo baba yao mzazi ni jirani yao tu hivyo hiyo kesi wamesingiziwa kwa kuwa Shija Kamuga anawivu na ndoa yao.
Upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo iwape adhabu kali washtakiwa hao ili iwe fundisho kwao na onyo kwa wengine wenye nia au lengo la kufanya kitendo walichokifanya washtakiwa, ukizingatia kuwa kitendo cha kujamiana ndugu wa kaka na dada na kuishi kama mke na mme pamoja kuzaa mtoto ni kitendo cha ajabu na cha aibu na kinyume cha maadili ya Kitanzania na Kiafrika kwa ujumla.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Maswa,Mhe.Azizi Khamis bila kuacha shaka yoyote kwa pande zote mbili ndipo akawahukumu kwenda kutumikia kifungo cha miaka 20 jela mshtakiwa wa kwanza ,Mussa Shija huku Hollo Shija akihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa makosa ya kujamiana ndugu wa damu kisha kuishi kama mke na mme na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume.