Sibuka FM
Sibuka FM
1 October 2025, 7:03 pm

Nimekuwa mkulima wa Pamba kwa muda mrefu sasa lakini zamani nilikuwa nalima kiholela sana hivyo sikupata mavuno mazuri Lakini baada ya kupata elimu sahihi na Ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo, mwaka huu nimepata kilo zaidi ya elfu tatu za Pamba kwa ekari moja Ninaishukuru sana Serikali kupitia Bodi ya Pamba Tanzania-TCB
Inaelezwa kuwa mkulima kupata zaidi ya kilo elfu tatu kwa ekari moja ni kama ndoto lakini imewezekana kwa mkulima Kusekwa Matonange kutoka Kijiji cha Nyansalala kata ya bukondo Wilaya ya Geita Mkoa wa Geita ambaye katika msimu huu kilimo wa 2024/2025 amepata Kilo zaidi ya elfu tatu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo mkulima huyo alipata zaidi ya kilo zaidi ya elfu mbili.
Mzee Matonange anaeleza siri za mafanikio katika mavuno hayo licha ya kupata changamoto za hapa na pale, lakini anasisitiza kufuata kanuni za kilimo cha pamba pamoja na ushauri anaopewa na wataalamu wa kilimo huku akitoa shukurani nyingi kwa Bodi ya Pamba Tanzania – TCB kwa jitihada zinazofanyika kwa lengo la kumuinua mkulima na kuongeza Uzalishaji
Elisha Athanasi ni kijana anayejishirikisha na zao la pamba huku akijifunza kutoka kwa mzee kusekwa Matonange anatoa wito kwa vijana kujikita katika zao hilo kwasababu kinainua wakulima kama watafuata kanuni na ushauri wa wataalamu wa kilimo

