Sibuka FM
Sibuka FM
1 October 2025, 8:11 am

“Kama mnavyojua wilaya ya Igunga inalima zao la Pamba na kuzalisha kitalu mbegu hivyo Serikali inafanya jitihada zote kuhakikisha uzalishaji unaongezeka mwaka hadi mwaka hivyo zao hili tunalipa kipaumbele kwasababu ni zao la kibiashara.” Sauda Mtondoo DC Igunga “
Na Nicholaus Machunda
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Mhe Bi Sauda Mtondoo ametoa maagizo kwa wakulima wa zao la Pamba kuhakikisha wanafuata kanuni bora za kilimo cha zao hilo ili uleta tija na kujikwamua kiuchumi.
Mhe Mtondoo ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira baada ya kumtembelea ofisini kwake ili kutaka kujua Wilaya yake imejipangaje katika uzalishaji Wenye tija katika zao la Pamba maarufu kwa jina la dhahabu nyeupe
Mhe Mtondoo ameongeza kuwa Wilaya ya Igunga tayari imeshapata mgao wa mbegu kwa ajili ya kilimo cha Msimu wa 2025/2026 hivyo kuwaondoa wasi wasi wakulima kuhusu upatikanaji wa mbegu huku akiishukuru Serikali na Bodi ya Pamba Tanzania kwa kuleta mbegu kwa wakati
Kwa upande wake afisa kilimo kutoka mradi wa Jenga kesho iliyo bora ( Buld Better Tommorow – BBT ) Nice Thomas amezungumzia ujio wa mbolea Ukaa inayotengenezwa kutokana na masalia ya miti ya Pamba inavyoweza kuongeza tija katika Uzalishaji wa Pamba

Baadhi ya wakulima waliozungumza na Sibuka Fm wamesema kuwa elimu ya mbolea ya Ukaa itaenda kuwaongezea Uzalishaji wa Tija huku wakiwaomba wakulima wenzao ambao bado hawajatoa masalia ya pamba watoe mapema ili kufanya maadalizi ya shamba kwa ajili ya kilimo cha pamba
