Sibuka FM
Sibuka FM
22 September 2025, 10:13 pm

Niingia madarakani nitafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi wa maji ya ziwa Viktori unakamilika maana utazifaidisha kata zangu za Zanzui, mwamashimba, Buchambi na kata ya Busangi ambazo zinachangamoto ya Maji ” Mashimba Ndaki -mgombea ubunge maswa magharibi -ccm “
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi lililopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Mhe Mashimba Mashauri Ndaki amezindua rasmi kampeni ili kuomba ridha ya wananchi huku akitaja vipaumbele atavyoanza navyo baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi utakaofanyika mwisho wa mwezi Oktaba , 2025
Mhe Mashimba anaomba kukutea nafasi yake kwa kipindi kingine ili aendelee kuwapambania hasa mradi wa maji kutoka ziwa viktoria ambayo ndio itakuwa mwarobaini ya changamoto ya maji katika Jimbo lake.
Aidha Mhe Mashimba amesema kuwa wakati anapata ubunge jimbo lilikuwa chini kimaendeleo hasa katika huduma za upatikanaji wa Maji baada ya kuingia alisimamia maeneo mengi yakapata maji na kupunguza adha waliyokuwa wanapata wananchi wake.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo ambae pia ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Maswa Mwl Onesmo Makota amesema kuwa chama kitafanya kampeni za kistaarabu bila vurugu wala ugomvi hivyo wananchi wakiamini ili kudumisha amani tuliyo nayo
Dkt George Lugomela ni Mgombea ubunge Jimbo la Maswa mashariki akapata nafasi ya kumuombea kura Mgombea ubunge Jimbo la Maswa Magharibi Mhe, Mashimba ndaki huku akisema wajumbe wa Maswa Magharibi hawakukosea kumchagua kwani ni mchapaka kazi na mfuatiliaji wa maendeleo kwa wananchi wake

