Sibuka FM
Sibuka FM
22 September 2025, 7:14 pm

Ujio wa kambi ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa utasaidia kusogeza huduma kwa wananchi ambazo walitakiwa wazipate katika Hospitali kubwa za rufaa na kanda lakini kwa sasa zinatolewa na Hospitali yetu ya Wilaya ” Dc Maswa Dkt Vicent Anney “
Wananchi wa Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za Madaktari bingwa zilizoletwa na Halmashauri ya wilaya kwa lengo kusogeza huduma za kibingwaa kwa wananchi
Wananchi hao wameishukuru serikali kwa uwepo wa huduma hizo za kibingwa kwenye Hospitali ya wilaya kwani hapo awali walikuwa wanatumia gharama kubwa kwenda hospitali na mikoa na za rufaa kwa ajili ya kupata huduma hizo

Dr Deogratius Mtaki ni Mganga mfawidhi katika Hospitali ya wilaya ya maswa amesema kuwa huduma zinazotolewa na Madaktari bingwa hao ni pamoja matibabu ya Macho, Masikio, Pua, Koo, Upasuaji mkubwa , upasuaji mdogo na huduma za Uzazi kwa wanawake
Aidha Dr Mtaki ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta vifaa tiba vya kisasa na kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi hivyo wananchi waitumie ili kupata huduma bora
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney amewataka wananchi wenye changamoto za afya wajitokeze kwa wingi ili kupata huduma za kibingwa huku akiupongeza uongozi wa Halmashauri kwa ubunifu huo wenye lengo la kusogeza huduma kwa wananchi

