Sibuka FM
Sibuka FM
15 September 2025, 5:52 pm

Nimekuwa serikalini kwa muda mrefu hivyo nina uzoefu wa namna ya kufuatilia na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Maswa Mashariki, ninachoomba wanipe ridhaa ya kwenda kuwasemea huko Bungeni ” Dkt George Lugomela “
Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi ccm Jimbo la Maswa mashariki lililopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Dkt George Venance Lugomela ameahidi kutatua changamoto za Maji, Afya, Elimu na Kilimo endapo atachaguliwa kuwakilisha wananchi kwa nafasi ya Ubunge,
Dkt Lugomela amesema wakati wa Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi zilizofanyika katika Kijij cha Ipililo, kata ya Ipililo Wilayani hapa na kusema kuwa kumekuwepo na changamoto nyingi ambazo ameziona hivyo anaomba ridhaa ya Wananchi ili akazitafutie ufumbuzi katika ngazi za juu za maamuzi
Aidha Dkt Lugomela amesema kuwa Serikali imefanya mambo makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Maswa Mashariki hivyo ameahidi kwenda kuendeleza yote yaliyoanzishwa ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati kuu ya ccm Taifa na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha ndugu Joshua Chacha Mirumbe amewataka wana ccm kuvunja makundi na kumnadi mgombea aliyepitishwa na chama katika Uchaguzi wa Rais, Wabunge pamoja na Madiwani
Shemsa Mohamedi ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Simiyu amewataka wanaccm na wananchi wa Maswa kuhakikisha wanaichagua ccm ili iweze kuleta maendeleo kwa Wananchi ifikapo tarehe 29. Oktoba, 2025
Nao baadhi ya makada wa ccm, Stanslaus Nyongo na George Mayunga wakapata nafasi ya kuzungumza na wana ccm na wananchi wa Ipililo na kumuombea kura mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Mashariki Dkt George Lugomela


