Sibuka FM
Sibuka FM
11 September 2025, 11:59 am

Mfumo huu wa NeST ni mzuri maana mchakato wake wa kupata mzabuni unafanyika kwa uwazi na haki hivyo niwasihi wana Maswa na vikundi vya wajasiliamali kujiunga katika mfumo huu ili waweze kunufaika na fulsa zinazotangazwa na halmashauri na taasisi zingine za manunuzi “Elnight Mmari -afisa manunuzi halmashauri ya wilaya ya Maswa “
Zaidi ya wajasiliamali 50 kutoka vikundi mbalimbali Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, wamepewa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo wa manunuzi wa Serikali –NeST pamoja na fulsa zinazopatika katika mfumo huo
Akizungumzia mfumo huo na fulsa zinazopatika, afisa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma –PPRA Bi, Glory Didas amesema kuwa vikundi vitakapojisajili katika mfumo huo watakutana na fulsa za Serikali zitakazowasaidia kuinuka kiuchumi na kuongeza pato la Taifa
Eveline Kapologwe ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- Tamisemi amesema mafunzo hayo kwa Makundi maalumu ya Vijana, Wanawake,Wazee na watu wenye Ulemavu yatasidia kutambua fulsa zinazotengwa na taasisi za manunuzi

Kwa upande wake afisa manunuzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bi, Elnight Mmari amesema mfumo huo wa NeST unafanyika kwa Uwazi na hauna upendeleo wowote wala kutoa Fedha kwa wanaoomba Zabuni hivyo akatoa wito kwa vikundi vya wajasiliamali kujiunga kwenye mfumo ili waweze kunufaika na fulsa zinazotolewa na Halamashauri
Baadhi ya wanavikundi walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamewaongezea uelewa katika mfumo wa manunuzi ya Umma na kutoa wito kwa makundi ya Vijana kuwa waaminifu katika marejesho ya fedha wanazokopa ili ziendelee kunufaisha vikundi vingine
Mafunzo hayo yametolewa kwa Wajasiliamali na Vikundi maalumu kwa kushirikiana na Idarai ya maendeleo ya Jamii, PPRA, Tamisemi na Tasisi ya WAJIBU


