Sibuka FM
Sibuka FM
23 August 2025, 3:37 pm

“Matukio ya wanyama pori wakali kuvamia makazi ya watu na kuua mifugo kuna kila namna ya kufanya kwa mamlaka za wanyama pori ili kuleta usalama kwa wananchi na mali zao lengo ni kuondoa umasikini kwa jamii kutokana na nguvu kubwa waliyoitumia hadi kuwa na mifugo”.
Na Anitha Balingilaki
Kundi la Fisi limevamia na kuua Kondoo 17,Mbuzi watano na wengine kujeruhiwa nyumbani kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasambo A kilichopo kijiji cha Gambasingu kata ya Nkoma halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Akizungumza na Sibuka Fm mwenyekiti wa kijiji cha Gambasingu,Buka Bulugu anaeleza namna alivyoshiriki kuwafukuza Fisi walioua mifugo ya mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasambo pale walipovamia Kondoo na Mbuzi.
Hatua hiyo imekuja ikiwa zimepita siku chache tangu fisi kuua na kushambulia kondoo na mbuzi nyumbani kwa Singisi Kija ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasambo “A”.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa,Singisi Kija mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasambo “A”, ambaye ndiye mmiliki wa Kondoo na Mbuzi zilizouliwa na Fisi anaeleza hali ilivyokuwa na hasara aliyoipata kutokana nguvu kubwa aliyoitumia kuwekeza kwenye mifugo hiyo.
Kwa upande wao Sitta Kija na Lucas Kikaja wakazi wa kijijini hapo wameomba mamlaka husika kuwa thibiti wanayama wakali ili wasiendelee kuleta maumivu kwa jamii.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kijiji cha Gambasingu,Buka Bulugu akatoa ushauri kwa jamii wa kujenga mabanda/mazizi imara ili kukabiliana na changamoto za wanyama hao.
Mfugaji huyo kabla ya tukio alikuwa na jumla ya mbuzi na kondoo 53.