Sibuka FM
Sibuka FM
4 July 2025, 4:18 pm

“Hakuna maendeleo ya vitu bila watu lazima tuendelee kutoa elimu ya usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini ili kupunguza au kumaliza matukio ya wachimbaji wadogo maana kila kukicha tunaona vifo,majeruhi na ulemavu wa kudumu hivyo mamlaka husika zinao wajubu mkubwa wa kuelimisha kuhakikisha usalama kwa wachangiaji wa pato la taifa”.
Na, Daniel Manyanga
Imeelezwa kuwa matukio ya ajali migodini taklibani 92 yameripotiwa nchini yaliyoweza kuua wachimbaji wadogo wa madini,kujeruhi na kuacha ulemavu wa kudumu kwa kipindi cha mwezi June 2024 hadi June.30.2025.
Hayo yamesemwa na mhandisi wa migodi nchini kutoka tume ya madini, Emmanuel Gisiri wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa sekta hiyo kutoka mikoa ya Simiyu na Mara katika mafunzo ya usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini yaliyofanyika mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Emmanuel Gisiri amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi June mwaka Jana hadi June 30.mwaka huu matukio ya ajali migodini yapatayo 92 yameripotiwa katika migodi ambayo yamesababisha vifo,kujeruhi na kuacha ulemavu wa kudumu kwa wachimbaji wa madini hali iliyosababishwa na elimu duni ya uchimbaji salama kwa watenda kazi.
Kwa upande wake kamishna wa tume ya madini mhandisi, Theonista Mwasha wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa sekta hiyo kutoka mikoa ya Simiyu na Mara katika mafunzo ya usalama kwa wachimbaji wadogo ambapo amewataka wachimbaji hao kuzingatia usalama wao wakati wakielezea majukumu pamoja na matumizi salama ya kemikali.
Mashauri Ntizu, Elias Mayala na Jason Saguda ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza namna ambavyo mafunzo hayo yatawasaidia kuwa salama katika shughuli zao za uchimbaji wa madini migodini.

