Sibuka FM
Sibuka FM
21 June 2025, 5:36 pm

“Tuendelee kuwakumba wenye uhutaji katika kurudisha faraja kutokana na familia hizo kupitia kwenye changamoto kwa kipindi hicho na hii ni ibada kubwa sana kwa Mungu wetu kwa kutoa sadaka kwa wenye changamoto mbalimbali”.
Na, Daniel Manyanga
Jamii wilayani Maswa mkoani Simiyu imekumbushwa kuzikumba familia zenye mahitaji maalum katika kurejesha furaha kutokana na changamoto mbalimbali inazopitia familia husika.

Ombi hilo limetolewa na mkurugenzi wa taasisi ya Juniors and Child Care Foundation (JACCAFO), Joseph Ngeleja Jidayi wakati akitoa msaada wa mahitaji mbalimbali muhimu kwa familia ya Bi.Anitha ya mjini Maswa iliyopata janga la kuungua kwa moto nyumba ambayo wanaishi mnamo tarehe 06.06.2025 majira ya saa saba usiku huku chanzo cha moto huo kikitajwa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye nguzo ya umeme.
Ngeleja ametoa shukrani kwa watu wote walioguswa kwa kutoa michango yao huku akitaja thamani ya vitu vyote vilivyotolewa kwenye familia hiyo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tukio la utoaji wa msaada huo katibu wa Juniors and Child Care Foundation (JACCAFO),Roseanna Sewangi amesema kuwa kama taasisi wataendelea kugusa jamii kadri ya uwezo wao ili kurejesha tabasamu kwa watu.
Masule Mboje na Anitha Tinya ni wanafamilia waliopatwa na janga hilo la moto wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwakumbuka katika kipindi hichi kigumu wanachopitia hivyo jamii iendelee kutoa msaada kutokana na wao kuhitaji msaada mkubwa kwa muda huu huku wakitaja thamani ya nyumba na vitu vilivyoteketea kwa moto ndani ya nyumba.

