Sibuka FM
Sibuka FM
18 June 2025, 9:43 pm

Hamasa ya ulimaji wa zao la Pamba wilayani Maswa mkoani Simiyu huenda ukaongezeka kufuatia ongezeko la uwekezaji wa viwanda vya kuchakata na kuchambua mali ghafi ya zao la Pamba mkoani hapa.
Na,Alex Sayi
Bank ya Eguity imejitanabahisha kufanya mapinduzi kwa kushiriki nakuchochea hamasa ya ununuzi wa zao la Pamba kwa bei yenye tija kwa wakulima wilayani Maswa mkoani Simiyu
Akizungumza na Sibuka fm wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania mkoani Simiyu Meneja wa biashara toka Bank ya Equity Mwanza(CPA)Emerald Landy Mutajwaa amesema kuwa Equity Bank wamefadhili mtaji kwa ajili ya shughuli za ununuzi wa zao la Pamba

Ham Ngaza mwananchi na mkulima mkazi wa Kijiji cha Ng’hami kata ya Nyalikungu wilayani Maswa mkoani hapa amesema kuwa ongezeko la bei linawanufaisha wakulima wa zao hilo
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Juni 18/2025 maeneo ya viwanja vya Nguzonane akiwa ziarani wilayani Maswa Mkoani hapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hasan amesema kuwa wakulima wa zao la Pamba wanapaswa kuendelea kuzalisha zao hilo kwa kuwa kwa sasa soko lipo
Aidha Mhe.Dkt.Samia amempongeza mwekezaji huyo huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa mwekezaji huyo nakumtaka mwekezaji huyo kuongeza uwekezaji