Sibuka FM
Sibuka FM
17 June 2025, 5:34 pm

Maelekezo ya Mh Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Wizara inatengeneza Mazingira mazuri ya Uwekezaji na ufanyaji Biashara
Imeelezwa kuwa zaidi ya ajira 350 za moja kwa moja kwa wazawa na zingine 800 zisizo za moja kwa moja zitazalishwa kutoka kiwanda cha kutengeneza na kuchakata pamba cha BIO-SUSTAIN kilichopo Wilayani Meatu Mkoani Simiyu
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe wakati wa Uzinduzi wa kiwanda hiyo na kusema kuwa kiwanda hicho kitaenda kuongeza fedha za kigeni na uzalishaji wa mafuta ya kula yanayotokana na mbegu za pamba
Mhe Kigahe amesema kuwa mipango ya Serikali ni kuhakikisha inaboresha mazingira ya Ufanyaji biashara na uwekezaji kwa wazawa ili kuleta tija kwa Taifa
Salum Halfan ni meneja wa kiwanda cha kuzalisha pamba amesema uwekezaji wa kiwanda hicho ni zaidi ya Bilioni 14 kikiwa na uwezo wa kuzalisha pamba mbegu na pamba nyuzi zaidi ya kilo laki 5 kwa siku
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe Leah Komanya amesema uwepo wa kiwanda hicho unaenda kuchochea ajira kwa wananchi huku kipaombele kikiwa ni wananchi wazawa wa Wilaya ya meatu na Mkoa wa Simiyu