Sibuka FM
Sibuka FM
17 June 2025, 8:34 am

“Tunapandisha zao moja baada ya jingine niseme tu kuwa zao la pamba ni wapo ya mkakati uliyopo katika kuleta uhalisia wa gharama anazotumia mkulima ili uchumi wa mtu mmoja mmoja na mkoa wa Simiyu uweze kukua na kuongeza hali ya wakulima kupenda kilimo hicho.”
Na, Nicholaus Machunda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt .Samia Suluhu Hassan ameahidi kupandisha hadhi zao la Pamba kwa sababu ni tegemeo kwa mkoa wa Simiyu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia zao hilo ambalo ni utambulisho wa mkoa huo.

Mhe.Dkt.Samia amesema hayo leo wakati akizindua kiwanda vya uchakataji wa Pamba na kiwanda cha kutengeneza bomba za maji vilivyopo katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mhe.Dkt.Samia amesema kuwa viwanda hivyo vyenye gharama ya shilingi bilioni 8 vinavyomilikiwa na kampuni ya Moli Oil Mills kampuni LTD Vitaenda kupandisha bei ya zao pamba na kuinua uchumi wa wana Simiyu.
Aidha katika hatua nyingine Mhe.Dkt.Rais Samia amempongeza mwekezaji wa ndani katika kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji kwani serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mabomba nje ya nchi hivyo itapunguza gharama ya kuagiza nje.

