Sibuka FM
Sibuka FM
16 June 2025, 2:40 pm

“Tuwalinde ,tuwapende ,tuwatimizie mahitaji ya msingi watoto wetu hii ni njia pekee ya kukomesha ukatili kwa watoto hivyo kumaliza changamoto ya watoto mitaani ambao baadae hujeuga na kuwa wezi,vibaka na chokoraa tukifanya hivyo kila mzazi au mlezi kwa nafasi yake hakuna sheria itakayo kufunga kwa kushindwa kuwapa haki za msingi watoto”.
Na, Daniel Manyanga
Jamii ya watoto wanaopata malezi ya kiroho na kimwili katika vituo vya huduma ya watoto na vijana ya Compassion International kluster ya Maswa mkoani Simiyu wameiomba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi,walezi na watu wanaowafanyia ukatili hali ambayo inawanyima haki zao za msingi.
Ombi hilo limetolewa na Marieth Abas na Neema Donald ambao ni watoto wanaopata huduma ya malezi ya kiroho na kimwili katika vituo vya huduma ya watoto na vijana wakati wa maadhimisho ya mtoto wa Afrika yalifanyika katika kanisa la AICT Majengo chini ya ufadhili wa shirika la Compassion International na kuhudhuriwa na wadau wa watoto.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema kuwa wazazi na walezi kutowasikiliza watoto na kutowatimizia mahitaji hao ya msingi ni moja vitu ambavyo vinawafanya watoto kukosa haki zao za msingi hivyo kuanza kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu ili kuweza kujikimu mahitaji yao ya kila siku.
Kwa upande wake mwenyekiti wa vituo vya huduma ya watoto na vijana kluster ya Maswa,Sandei Sarara amesema kuwa moja ya malengo mama ya shirika la Compassion International ni kuwaondolea umasiki watoto kiroho na kimwili kwa kuwawezesha kupata ujuzi mbalimbali utakaoweza kuwasaidia pindi wanapokuwa watu wazima.
Maadhimisho ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka inapofika mnamo tarehe 16.06 ya kila mwaka ikiwa ni kuwakumba watoto waliouliwa na makaburu katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini wakati wanapigania haki zao kutoka kwa wazungu huku kaulimbiu ya mwaka huu “Haki za mtoto,Tulipotoka,Tulipo na Tuendako”

