Sibuka FM
Sibuka FM
5 June 2025, 9:15 am

Diwani ni haki yake kufanya biashara ya Ununuzi wa Pamba kwasababu pamba siyo shughuli ya Halmashauri kwahiyo hakuna mgogoro wa kimasirahi kwa diwani kununua Pamba, Lakini sitavumilia Diwani atakayefanya hujuma katika ununuzi wa Pamba mimi Nitakuning’iniza tu “Mhe Dkt Vicent Anney -Mkuu wa Wilaya ya Maswa “
Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu wametahadharishwa kuhusu Figisu wanazofanya katika Ununuzi wa zao la Pamba na kusema kuwa hatawavumilia wale watakaofanya Ununuzi halafu wakafanya udanganyifu wa kuibia Wakulima
Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe, Dkt Vicent Naano Anney wakati akitoa Salamu za Serikali katika Kikao cha Baraza la Madiwani liliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo na kusema ni haki ya Diwani kununua Pamba lakini lazima atimize sheria, Taratibu na wajibu wa ununuzi wa pamba
Aidha Dkt Vicent Anney amewatahadharisha Viongozi wa Amcos wanaochezea Mizani kwa lengo la kuwaibia wakulima na kusema mizani ya sasa ina Mfumo ya kisasa ambayo inamwezesha Mkuu wa wilaya, Bodi ya Pamba na Wizara ya Kilimo kuona mwenendo wa ununuzi wakiwa Ofisini kwao
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe, Paul Maige ameishukuru Serikali kwa kuleta Fedha nyingi kwa ajili ya Shughuli za Maendeleo huku akisema Makusanyo yameongezeka hadi kufikia asilimia 79 kulingana na Malengo waliyojiwekea katika mwaka wa fedha 2024/2025

Naye Mbuge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo lake amemshukuru Rais Samia kwakuleta miradi kila kata na kuziomba taasisi ambazo zinatekeleza miradi ya Maendeleo kukamilisha kwa Wakati ili wananchi wanufaike kama ilivyokusudiwa
Kwa upande wake wenyekti wa Chama cha Mapinduzi ccm Wilaya ya Maswa Ndugu Onesmo Makota amesema kuwa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu 2025 tuendelee kudumisha Amani ili uchaguzi ufanyike salama na kumalizika Salama huku akiwataka Viongozi na watendaji kuzitatua changamoto ambazo zitaleta vikwazo vya Ushindi wa chama hicho.