Sibuka FM
Sibuka FM
4 June 2025, 8:25 pm

“Rushwa ni adui wa haki na maendeleo lazima kwa nguvu zote viongozi waipinge rushwa maana leo utaona kuna watu wachache wasiokuwa waadilifu wanatumia turufu ya uongozi wao kupora haki za watu kujilimbikizia mali ambazo ni wizi na kuwanyima watu ambao walistahili haki zao kwa kuwa tu mkono mtupu haulambwi.”
Na, Daniel Manyanga
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu imepokea malalamiko tisa ya vitendo vya rushwa kutoka kwenye vyama mbalimbali vya ushirika Amcos mkoani hapo katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi sasa huku milioni ishirini na sita zikiliwa na viongozi wa ushirika wasiokuwa waadilifu.
Akizungumza na Sibuka Fm mwakilishi wa kamanda wa TAKUKURU mkoani hapa, Peter Mkombe wakati akitoa elimu ya masuala ya rushwa kwenye jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoani hapa lililofanyika wilayani Itilima na kuongeza kuwa viongozi wachache wa ushirika wananufaika wao hivyo ni vyema wakawa waaminifu ili kuepuka kukutwa na sheria kali za uhujumu uchumi.
Akizungumza kwenye jukwaa hilo,Godfrey Mpepo mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu amesema sheria za ushirika zipo vizuri sana hivyo hakuna kiongozi yeyote aliyeko juu ya sheria lazima wafanye kazi kwa kufuata miiko ya uongozi na kuzingatia viapo vyao.

Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Itilima ,Polycarp Ntapanya amewata viongozi wa AMCOS kusimamia na kuzingatia maadili ya kazi zao.
