Sibuka FM
Sibuka FM
12 May 2025, 1:05 pm

‘‘Kuchangia uchumi wa nchi kupitia utalii siyo jukumu la watilii wa kigeni kama ambavyo watu wengine wanafikiri sote tunajukumu hilo kama wananchi wazalendo ambao tunazunguka katika maeneo ya hifadhi au mapori ya akiba ili sisi tuwe mabalozi wazuri hata kuwajuza huko nje kuwa hata sisi wa ndani tunafanya kazi ya kujionea vivutio mbalimbali na kuchangia pato la taifa’’.
Na,Daniel Manyanga
Wananchi waishio maeneo yanayozunguka Pori la akiba Kijereshi lililopo katika wilaya za Bariadi na Busega mkoani Simiyu, wameaswa kujijengea desturi ya kufanya utalii wa ndani ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika pori hilo na kuchangia pato la taifa kupitia sekta ya utalii na siyo kuwaachia tu watalii kutoka nje ya nchi kujionea vivutio na kuchangia pato la taifa.

Akizungumza na Sibuka Fm wakati wa uzinduzi wa msimu wa utalii kwa mwaka 2025 uliofanyika katika pori la akiba Kijereshi na kuwakutanisha wananchi wa maeneo mbalimbali yanayolizunguka pori hilo,mkuu wa kituo cha polisi Lamadi, Mrakibu wa polisi, Emanuel Shani amewataka wananchi hao kuendelea kulilinda pori hilo pamoja na kujitokeza kufanya utalii wa ndani ili mapato yanayopatikana yaweze kutumika katika kukuza uchumi wa taifa.
Kwa upande wao maafisa wahifadhi wa pori la akiba la Kijereshi,Adelald Tesha afisa utalii na Mohamed Mpita afisa mhifadhi kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) wameeleza fursa zitakazopatikana kupitia msimu huo wa utalii uliozinduliwa.
Tumaini Patrick na Nyamburi Moshi ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki uzinduzi wa msimu wa utalii wameleeza vivutio walivyoviona katika pori hilo, huku wakiwahamasisha wananchi wengine kuendelea kujitokeza kufanya utalii wa ndani ili kujionea vivutio pamoja na kuchangia pato la taifa kupitia utalii wa ndani.