Sibuka FM
Sibuka FM
4 May 2025, 9:29 pm

Ukanda huu wa Wilaya za Maswa na Meatu unachangamoto ya kuwa na Maji ya Chumvi hivyo nitatuma wataalamu waje kufanya utafiti wa namna ya kupata maji Mazuri maana kwa sasa Wizara ya Maji ina Mitambo ya kisasa “Dkt George Lugomela “
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji Dkt George Lugomela ameahidi kutuma wataalamu kwa ajili ya kuja kufanya utafiti kuhusu upatikanaji wa Maji baridi katika maeneo ambayo yanachangamoto ya upatikanaji wa Maji ya chumvi.
Dkt Lugomela amesema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Maswa na kusema kuwa Wizara itatuma wataalumu pamoja na Mitambo yenye teknolojia ya kisasa itayosaidia kubaina sehemu za Maji mazuri yatakayosaidia wananchi wa Maswa na Maeneo mengine
Aidha Dkt Lugomela amemshukuru Mhe Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya Maji pamoja na Ujenzi wa Mabawa hasa katika Maeneo yenye hali ya Ukame ikiwemo Mkoa wa Simiyu ili kuondoa changamoto ya huduma ya Maji huku akiwahakikisha wananchi wote waliotoa maeneo yao kwa ajili ya Ujenzi wa mabawa watalipwa fidia zao

George Itumbula ni Mhandisi Ujenzi bonde la ziwa Victoria amesema kuwa wote waliotoa maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Bwawa la Ipililo tayari wameshalipwa fidia zao isipokuwa wachache ambao hawakuwepo kwenye utaratibu wa awali na kuahidi kulifanyia kazi ili nao walipwe stahiki zao.
Awali akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa rasilimaji Maji Wizara ya Maji Dkt George Lugomela , Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini –RUWASA Wilayani Maswa Mhandisi Lucas Madaha amesema kuwa kukamilika kwa mabawa hayo yatasaidia kuongeza Upatikanaji wa huduma ya Maji kwa Wananchi
Baadhi ya Wananchi kutoka kata ya Ipililo wilayani Maswa wameishukuru Serikali ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan pamoja na Dkt Lugomela kwa kuwakumbuka wananchi wa Ipililo na Maeneo mengine kwani Maji ni Uhai na yanahitaji kila sehemu.

