Sibuka FM
Sibuka FM
1 May 2025, 5:47 pm

“Jumuiya ya wafanyabiashara(TTCIA)wilayani Maswa mkoani Simiyu wameonya nakutotaka jina lao kutumiwa na watu kwa maslahi yao binafsi,hali inayowachonganisha wao na watendaji wa Serikali Wilayani hapo”.
Na,Alex Sayi-Maswa Simiyu
Jumuiya ya wafanyabiashara wilayani Maswa mkoani Simiyu(TTCIA) wamekanusha taarifa zilizotolewa mitandaoni kwenye tovuti ya Jamii foram April,28/2025 saa 03:56 asubuhi,wakilalamika kuchangishwa fedha kinyume cha utaratibu kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Maswa aliyehamishiwa kutoka wilayani Bunda mkoani Mara.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wafanyabiashara hao wakiwa kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo wakati wakiwasilisha walaka wa kanusho lao hilo April.30 mwaka huu
Akiwasilisha waraka huo wa kanusho kwa mkuu wa wilaya hiyo,mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara wilayani Maswa mkoani Simiyu ,Winfrida NJige amesema kuwa taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na kichwa cha habari kilichosomeka”Maombi ya uchunguzi kuhusu uchangishaji fedha kinyume na taratibu kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Maswa’‘ hazina ukweli wowote.
Akizungumza na Sibuka fm Boniphace Mabonesho mfanyabiashara wa duka wa bidhaa mchanganyiko wilayani hapa amesema kuwa taarifa za kuchangishwa fedha kinyume na utaratibu kwa ajili ya ukarabati wa makazi ya mkuu wa wilaya ya Maswa hazina ukweli.
Kwa upande wake, Joseph Bujenja mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi ambae ni mjumbe wa (TTCIA) wilayani hapa amesema kuwa taarifa zilizoenea mitandaoni juu ya wafanyabiashara kuchangishwa fedha na katibu tawala wilaya ili kufanikisha ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Maswa kwake ni za uongo maana hajawahi kufikiwa na kuombwa mchango wa ukarabati wa nyumba hiyo
Benjamini John mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi akizungumza na Sibuka fm amesema kuwa taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ni uongo mtupu kama kuna mtu anataka kuwachafulia uhusiano wao na serikali ya wilaya hiyo basi aende kwingine lakini siyo wafanyabiashara
Ikumbukwe kuwa sakata hili linajili kufuatia mabadiliko madoko yaliyofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyopelekea mabadirishano ya ofisi kati ya Aswege Kaminyoge aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Maswa aliyehamishiwa wilayani Bunda, akikabidhi ofisi Feb,26/2025 kwa Dkt Vicent Anney aliyekuwa mkuu wa wilaya Bunda.