Sibuka FM
Sibuka FM
30 April 2025, 9:08 am

Niwaagize wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya Maji katika Wilaya hii waongeze Kasi ili Wananchi wapate huduma ya Maji kama Serikali ilivyokusudia kusogeza huduma karibu na Wananchi Pia nitoe Onyo kwa Wananchi wanaoharibu Miundombinu ya Maji waache mara moja kwani tutawakamata na uwachukulia hatua “ DC Maswa Dkt Vicent Anney
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu Mhe Dkt Vicent Naano Anney amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya Maji katika wilaya hiyo kuhakikisha wanaongeza kasi katika utekelezaji wake ili wananchi wapate huduma kama ilivyokusudiwa
Mhe Anney amesema hayo wakati wa Ziara yake ya Kushutukiza katika Miradi mbalimbali ya Maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA) huku akitoa Onyo kali kwa baadhi ya Wananchi wanaoharibu Miundombinu ya Maji ikiwepo kukata Mabomba na kusababisha adha kwa watumiaji wa huduma hiyo
Aidha Dkt Anney amemshukuru Mhe , Dkt Samia Suluhu Hasan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa Wananchi wa Mji wa Maswa na maeneo jirani

Leonard Mnyeti ni Meneja ufundi wa MAUWASA amesema kuwa miradi hiyo inaenda kutatua changamoto ya Upatikanaji wa Maji katika Mji wa Maswa na Maeneo jirani yanayohudumiwa na Mamlaka hiyo
Mnyeti amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafanya huduma ya Maji ipatikane Saa 24 tofauti na sasa huduma inatolewa saa 16 huku akitoa wito kwa wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu katika chanzo hicho cha Maji kuacha mara moja ili bwawa liendelee kuhudumia wananchi wetu wa Maswa
Monica Deus Tubi ni Mkazi wa Kijiji cha Dodoma kata ya Buchambi Wilayani Maswa amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kusogeza huduma ya Maji safi tofauti na hapo awali walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta huduma ya Maji badala ya kufanya shughuli za kuwaletea maendeleo

